Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BOT YAZIUNGANISHA PAMOJA BENKI YA POSTA NA TWIGA

Benki Kuu ya Tanzania BoT, imeridhia uamuzi wa kuiunganisha Benki ya Twiga Bancorp Ltd na ile ya Tanzania Postal Bank Public limited Company (TPB Plc), ili iwe benki moja yenye nguvu ambayo utendaji wake utakuwa chini ya usimamizi na uendeshaji wa TPB Plc, uamuzi ambao utaanza Mei 17, 2018.


Hayo yamebainishwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt. Bernard Kibese wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mei 16, 2018 na kusema benki hiyo ya Twiga Bancorp iliyokuwa chini ya usimamizi wa benki kuu kwa takribani ya miaka miwili, ambapo mali za wateja na madeni ya benki hiyo kwa sasa yatasimamiwa na benki ya Tanzania Postal Bank Public Limited Company.

Dkt. Kabesema amesema uamuzi huu umechukuliwa ili kuboresha uangalizi na utendaji wa benki zinazomilikiwa na serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.

Pamoja na hayo, Naibu Gavana Kibese amesema hatua kama hiyo itachukuliwa pia kwa benki nyingine za serikali ambazo ufanisi wake hautokuwa wa kuridhisha, kwani nia ya serikali ni kuwa na benki moja kama sio chache zinazofanya vizuri, malengo ambayo Rais Dkt John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza mara kwa mara.

Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana, Bi Rosemery Tenga amewataka walikuwa wateja katika benki ambazo zipo chini ya BOT kufuata mitaji ya benki hiyo kuyumba kwenda katika benki hizo na utaratibu wa malipo utafanyika chini ya usimamizi wa bodi ya Amana.

Uamuzi huo wa BoT umetokana na benki ya Twiga kuwa na upungufu mkubwa wa mtaji ambapo ni kinyume na matwaka ya sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 na kanuni zake ambapo kwa wakati huo ilihatarisha usalama wa sekta ya fedha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com