Mbunge wa Buyungu (Chadema), Kasuku Bilago amefariki dunia leo Jumamosi Mei 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema: “Ni kweli amefariki dunia dakika 40 zilizopita, alikuwa amelazwa wodi ya Sewahaji."
Kuhusu chanzo cha kifo chake, Mbowe amesema:"Kwa sasa si wakati wake, tunahangaika kuhamisha mwili kutoka wodini kwenda chumba cha kuhifadhia maiti. Hayo mengine itakuwa baadae".
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Habari wa chama hicho, Tumaini Makene amesema taarifa zaidi zitatolewa baadaye na chama hicho.
Bilago alishiriki baadhi ya vikao vya Bunge la bajeti lililoanza Aprili 3, 2018 mjini Dodoma.
Social Plugin