Imeelezwa kuwa shambulio la aibu kwa mwanamke sio tu kupiga kelele
dhidi yake au kumgusa bali hata kumkonyeza pekee ni lugha ya ishara
inayoweza kukupeleka kuenda jela endapo ushahidi ukithibitika.
Mara
baada ya kuibuka mjadala uliozua gumzo mitandaoni kuhusiana na
shambulio la aibu dhidi ya wanawake eatv.tv ilimtafuta mwanasheria ili
kupata ufafanuzi kuhusu shambulio hilo ambapo, Wakili wakujitegemea
Johanes Konda amesema kwamba wanawake wengi hawatambui kama kukonyezwa
bila ridhaa yao ni kosa kisheria.
"Kanuni za adhabu sura ya 16 ndio inaelezea zaidi kuhusiana na shambulio la aibu lakini kulingana na mazingira na tamaduni zilizopo sasa, dada zetu wanaona kawaida tuu lakini sheria imewekwa kwa ajili ya kuwatetea wao dhidi ya shambulio hilo ambalo linaweza kuwa ni kwa kuguswa au kwa ishara kama kukonyeza au kupiga kelele za kuashiria kuna kitu cha tofauti kimepita", amesema Wakili Konda.

Wakili Konda amesema kuwa endapo wahusika ambao ni wanawake
wakizitambua haki zao na kuwashitaki watuhumiwa wanaweza kusaidia
kuondoa tabia hizo na endapo ikithibitika basi adhabu yake ni kuanzia
miaka isiyozidi 10 kushuka chini.
Hivi karibuni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa mjini Magharibi Kamishna
Msaidizi Mwandamizi Hassan Nassir amesema ni marufuku kukohoa pale
unapopishana au unapomwona mwanamke mwenye makalio makubwa kwamba
kukohoa huko kutapelekea kukamatwa kwa maana kitendo hicho ni 'shambulio
la aibu”.
Social Plugin