Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey PolePole amefunguka na kudai hajapokea taarifa zozote za kujiuzulu Katibu mkuu Taifa wa chama hicho, Abdulrahman Kinana kama zinavyoenezwa katika mitandao ya kijamii.
Polepole amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na eatv.tv alasiri ya leo Mei 27, 2018 baada ya kuenea uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa ndg. Abdulrahman Kinana ameandika barua rasmi ya kujiuzuli nyadhfa zake anazozishikilia ndani ya CCM.
"Taarifa kama hiyo huwa haitokagi kienyeji bali hutoka nje baada ya vikao kufanyika. Mimi ni mtu mdogo kwenye chama cha Mapinduzi kuelewa jambo kama hilo nje ya vikao. Ninachojua mimi Katibu Mkuu hajaniambia habari yoyote kuhusu kujiuzulu", amesema Polepole
Chanzo-EATV
Social Plugin