Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KINANA AMKABIDHI RASMI OFISI KATIBU MKUU MPYA WA CCM DKT. BASHIRU

Katibu Mkuu mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amemkabidhi nyaraka kama ishara ya kumkabidhi rasmi ofisi Katibu Mkuu mpya wa chama hicho Dkt. Bashiru Ali katika ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam leo Alhamis Mei 31,2018.

Kinana aliomba kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na kuitumikia kwa muda mrefu na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa alimkubalia na kumpendekeza Bashiru ambaye alipitishwa na Kamati Kuu ya CCM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com