Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Heshima ‘Chairperson Emeritus’ wa Bosi ya South Centre.
South Centre ni jumuiya iliyoundwa kwa makubaliano ya serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuchochea maendeleo katika nchi hizo.
Jumuiya hii iliundwa kwa makubaliano na ilianza kazi Julai 31, 1995 huku makao yake makuu yakiwa Geneva, Switzerland.
Kazi yake kubwa ni kusimamia maendeleo ya kiuchumi kwa nchi za kusini.
Hii hapa barua ya uteuzi aliyoandikiwa Rais Benjamin Mkapa.
Social Plugin