Kiev, Ukraine. Mwanahabari mashuhuri wa Urusi na mkosoaji wa utawala huo wa Kremlin ambaye iliripotiwa kwamba ameuawa nchini Ukraine, ameonekana akiwa hai katika mkutano wa waandishi wa habari ulioonyeshwa kwenye televisheni.
Iliripotiwa mapema kwamba Arkady Babchenko alikuwa ameuawa kwenye chumba chake katika jiji la Kiev, Ukraine. Lakini katika hali iliyoshangaza alionekana akiwa na maofisa usalama wa Ukraine katika mkutano uliotangazwa mubashara kwenye televisheni Ukraine.
Vyombo vya usalama vya Ukraine vilidai kwamba kifo chake kilifanyiwa operesheni ya uigizaji.
Kupitia akaunti ya Twitter, usalama ulisema ulipokea onyo la awali kuhusu jaribio la kuuawa kwa Babchenko na ukaamua kufanya operesheni ya kukusanya ushahidi wa kufanyika kwa shambulio la kigaidi na kikosi maalumu cha Urusi katika ardhi ya Ukraine.
Mapema, shirika la habari la serikali ya Ukraine la Ukrinform liliripoti kwamba Babchenko, 41, aliuawa kwa kupigwa risasi mgongoni na alifikia kwenye gari la wagonjwa na kutawaja walionusurika kuwa ni rafiki yake na msimamizi Ayder Muzhdabaev, naibu meneja mkuu wa Televisheni ya Ukraine.
Polisi mjini Kiev wanasema mke wa Babchenko alimkuta mumewe nje ya nyumba yao. Haikuweza kufahamika kama mke wa Babchenko na rafiki yake walikuwa wanajuwa kuhusu operesheni ya vyombo vya usalama.
Social Plugin