Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewapongeza
Wabunge kwa kuvaa Kanzu kwa wingi na kwa Wabunge wa Kike kuvaa Hijab.
Spika
ametoa pongezi hizo leo, Mei 18 mapema katikati ya kipindi cha maswali
na Majibu kwa serikali ambapo pia amemsifia Naibu Spika wa Bunge kwa
kuvaa Baibui na Hijab.
“Wabunge
kama hatujaendelea nimefanya utafiti wangu leo watu wengi sana
wamependeza kwa kuvaa Kanzu na kofia hongereni sana, tukumbuke tu kanuni
tunapo vaa tunatakiwa ivaliwe vilevile kama inavyovaliwa Pwani na miguu
sio kuvaa kiatu cha kamba hapana unavaa kobazi,” amesema Spika Ndugai
huku akicheka na Wabunge wakimpigia makofi.
“Lakini
kwa upande wa kina mama leo Hijab zimekubali, lakini katika Hijab,
Hijab namba moja leo hii ni ya Naibu wangu Mh. Naibu Spika, Mh. Naibu
Spika ebu simama kidogo hapo ahsante sana, hiyo inaonyesha Utanzania
wetu sisi ni wamoja,” ameongeza Spika.
Social Plugin