SERIKALI YATAJA SASABU ZA WABUNGE WA VITI MAALUM KUTOSHIRIKI VIKAO VYA FEDHA

Serikali imesema wabunge wa Viti Maalum hawaingii katika vikao vya kamati za fedha za halmashauri wanazotoka kwa sababu ya kutotajwa kwenye sheria iliyoainishwa na kifungu cha 41(1) na kifungu cha 40 (2)cha kanuni za kudumu za Serikali za Mitaa.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda ameliambia Bunge leo Mei 16, 2018 kuwa kanuni za Serikali za Mitaa za mwaka 2014, zinafafanua mahitaji ya sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka ya wilaya) sura 287, kifungu cha 75 na sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za miji) sura ya 288 kifungu cha 47.


Kakunda ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum (CCM), Taska Mbogo aliyehoji kwa nini wabunge wa viti maalum hawaingii kwenye vikao vya kamati za fedha za halmashauri zao.


Katika ufafanuzi wake, Kakunda amesema kamati ya fedha, uongozi na mipango imeundwa kwa mujibu wa sheria na inawataja wajumbe kuwa ni meya au mwenyekiti wa halmashauri ambaye atakuwa ni mwenyekiti.


Wengine ni naibu meya au makamu mwenyekiti, mbunge au wabunge wa majimbo, wenyeviti wa kamati za kudumu na wajumbe wengine wasiozidi wawili.


Amesema kwa sasa utaratibu utaendelea hivyo ikiwemo kutokutoa fedha za mfuko wa jimbo kwa wabunge wa viti maalum hadi hapo sheria itakapobadilishwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post