Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TFF YATAJA SABABU ZA MSINGI KUMUALIKA RAIS MAGUFULI ILI AKAWAKABIDHI SIMBA KOMBE



Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF) limeeleza sababu za msingi zilizowafanya kumualika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kama mgeni rasmi katika mchezo wa ligi kati ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar.

TFF imemualika Rais Magufuli kwa lengo la kuwakabidhi Simba taji la Ligi Kuu Bara walilolitwaa msimu huu wa 2017/18 pamoja na kukabidhiwa Kombe la CECAFA (U17) ambalo Serengeti Boys walifanikiwa kushinda huko Burundi.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, ameeleza kuwa sababu za kumualika Dkt. Magufuli ni kuongeza hadhi ya mchezo wa soka la Tanzania pamoja na wadhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kidao ameeleza kuwa unapomwalika mtu kama Rais wa nchi katika tukio unakuwa unapata fursa ya kuikiongezea kitu thamani kubwa akifananisha na mchezo wa soka la Tanzania namna utakavyopata heshima kubwa kutokana na ugeni rasmi wa Rais.

Mechi hiyo ya Simba na Kagera itaanza majira ya saa 8 kamili za mchana katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumamosi ya wiki hii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com