Taasisi ya Twaweza leo May 17, 2018
imetoa utafiti wake kuhusu masuala ya elimu ambapo imebainika kuwa
mitazamo ya wananchi kuhusu elimu bure imebadilika kwa kiasi kikubwa
ndani ya miaka 12 iliyopita.
Meneja Utetezi wa Twaweza, Anastazia
Lugaba amesema kuwa asilimia 87 ya watanzania kupitia utafiti huo kwa
mwaka 2017 uliopewa jina ‘Elimu bora au Bora Elimu? waitakayo watanzania’
wapo tayari kulipia ili kupata ubora kwenye elimu tofauti na mwaka 2005
ambapo (56%) ya wananchi walisema kuwa ni bora elimu itolewe bure kwa
watoto hata kama kiwango cha elimu ni cha chini.
“Tunaelewa
kwamba tumeelekeza watoto wapate elimu bure, japo tumeondoa michango na
pia tumeondoa ada lakini changamoto kwenye sekta ya elimu zinaonekana
kuwa ni nyingi na kubwa sana, kwasababu walimu ni wachache na wanafunzi
ni wengi sana” amesema Lugaba
Taarifa ya Twaweza inaeleza kuwa
matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa
1,789 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara pekee.
Social Plugin