Vijana 11 raia wa Tanzania waishio Johannesburg, Afrika Kusini walioshtakiwa kosa la ubakaji wameachiliwa huru na hakimu mkazi wa Mahakama ya Johannesburg.
Walikuwa wameshtakiwa kwa makosa ya kumteka nyara na kumbaka mwanamke mjamzito Thelma Mondowa raia wa Zimbabwe mwaka uliopita.
Waliachiliwa huru na Jaji Metisie kwa kukosekana kwa ushahidi.
Wakili wa upande wa mashtaka wa serikali alikuwa amemfahamisha hakimu kuwa Bi Thelma Mondowa aliamua kurejea Zimbabwe na wameshindwa kupata anwani yake.
Mwanamke huyo iliarifiwa alikuwa akitoka kazini na mfanyakazi mwenzake wa kiume pale ghafla walipovamiwa na kundi la wanaume wenye silaha na wakamvuta mwanamke huyo kabla ya kumpiga mfanyakazi mwenzake ambae baadaye alifanikiwa kutoroka.
Kisa hicho kilitokea mnamo 15 Mei mwaka 2015 katika barabara ya 270 Lilian Ngoyi mjini Johannesburg.
Baada ya mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu polisi na wakafanikiwa kufika eneo la tukio na kuwakuta wanaume hao wakimbaka kwa zamu mwanamke huyo.
Polisi wapatao kumi waliingia kwenye jengo ambapo tukio lilidaiwa kufanyika na kumuokoa mwanamke huyo na kumpeleka hospitalini.
Chanzo- BBC
Social Plugin