Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, ajira na watu wenye ulemavu Mh.
Antony Mavunde amesema kuwa Serikali inatambua kuwa wahitimu wa Elimu
ya juu ni wengi kuliko mafasi za ajira.
Waziri
Mavunde ametoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la Hadija
Ally Mbunge viti maalum (CCM) lililohoji serikali imepanua fursa kwa
kuongeza vyuo vikuu nchini, je ni kiasi gani mfuko wa vijana unaweza
kuwanufaisha walengwa ikizingatiwa kuwa tatizo la ajira ni hali halisi
inayowakabili vijana.
Mavunde amesema “Nafasi za ajira zinazotengenezwa kwa mwaka zimekuwa
ni chache kuliko wingi wa vijana hivyob basi serikali imeanza kuwabadili
mitazamo kuwa sio wote wanaoweza kukaa maofisini bali wanaweza kutumia
uwezo wao na kujiajiri katika sekta za kilimo na shughuli nyingine
halali zinazoweza wapatia kipato”.
Waziri mavunde ameongeza kuwa Mfuko wa Maendeleo ya vijana umeweza
kufikia vikundi 397 ambapo zaidi ya Bilioni nne zimekwisha tumika
kuwezesha vijana kiuchumi.
Social Plugin