Wanafunzi wawili wamekufa maji baada ya kivuko walichokuwa wakitumia kuzama katika eneo la Chulwi wilayani Mkuranga mkoani Pwani, huku watu wazima 10 wakiokolewa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Ali Hengo aliye eneo la tukio amesema wanafunzi hao walikuwa wakivuka kwenye kivuko ambacho sio rasmi wanachokitumia kila siku kwa ajili ya kwenda shuleni huku wakiwa na wananchi wengine, ambacho ndiyo kimezama na kusababisha vifo hivyo.
"Kuna watu walikuwa wakivuka pamoja na wanafunzi sasa wakazama, baada ya kuzama watu wazima waliokolewa lakini wanafunzi wawili, mmoja amekutwa amekufa mwingine amezama kwenye maji na hajulikani alipo, amesema Ali Hengo.
Ali ameendelea kuelezea hali halisi ya eneo hilo na kusema kwamba ..."Hiyo sehemu kuna kivuko watu wanavuka kienyeji sasa wanatumia mipira ya matairi ya gari ama miti kutengeneza tengeneza kama vingalawa tu vidogo vya kuvuka, sasa kutokana na mvua iliyonyesha ndio zikasababisha madhara haya".