Wazee wa klabu ya Simba wamemuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli
awapeleke wakaguzi wa mahesabu ndani ya klabu hiyo ili waweze kukagua
masuala ya mahesabu pamoja na kupitia sheria mbalimbali ambazo kwa namna
moja ama nyingine zimekaa kibaguzi katika michezo.
Tamko
hilo la wazee hao limetolewa leo Mei 18, 2018 zikiwa zimebakia siku
mbili kutoka sasa kufanyika kwa mkutano mkuu wa mabadiliko ya kikatiba
ndani ya Simba jambo ambalo limeonekana wazee hao kulipinga na kudai
mkutano huo ni batili kwasababu viongozi wa klabu hiyo wamekwisha
ibadili Katiba wao peke yao na wanachotaka ni wanachama sio mawazo yao.
Mbali na hilo, wazee hao wameendelea kupiinga rasimu ya Katiba ya klabu hiyo toleo la mwaka 2016 wakidai imepitishwa kinyume na sheria za nchi huku wakitaka itambulike Katiba ya mwaka 2014.
Mbali na hilo, wazee hao wameendelea kupiinga rasimu ya Katiba ya klabu hiyo toleo la mwaka 2016 wakidai imepitishwa kinyume na sheria za nchi huku wakitaka itambulike Katiba ya mwaka 2014.
Msilize hapa chini mwandishi wetu Crispin Haule 'Kiberenge' akielezea vizuri sakata hilo la wazee wa Simba lililotokea leo.
Social Plugin