Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JE SENEGAL KUIBEBA AFRIKA 16 BORA KOMBE LA DUNIA LEO??


Nafasi nyingine kwa Afrika kujaribu bahati ya kufuzu hatua ya 16 bora kwenye michuano ya kombe la dunia Urusi ambapo Senegal leo itakuwa na kazi ngumu dhidi ya Colombia.

Timu hizo za kundi H kila moja inawania ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua hiyo. Timu tatu kati ya nne za kundi hilo zote zina nafasi ya kufuzu hatua hiyo endapo zitashinda mechi zake, vinara Japan wanalingana pointi na Senegal wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo, wote wana pointi nne na Colombia ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu na Poland inashika mkia ikiwa haina pointi. Senegal ama ishinde mechi hiyo au ipoteze kwa zaidi ya bao, hiyo ndiye rekodi ambayo Simba hao wa Teranga watafurahia kuivunja.

Colombia haijawahi kupoteza mechi dhidi ya timu ya Afrika katika muda wa kawaida kwenye kombe la dunia. Walitolewa kwenye michuano hiyo na Cameroon mwaka 1990, lakini ilikuwa katika muda wa nyongeza. Mechi zao nyingine dhidi ya timu za Afrika zilimalizika kwa mafanikio, ikiifunga Tunisia bao 1-0 mwaka 1998 na kuifunga Ivory Coast mabao 2-1 mwaka 2014.

Kama Colombia itashindwa kupata matokeo dhidi ya Senegal, itakuwa ni mara ya kwanza kushindwa kuingia hatua ya mtoano ya michuano katika awamu mfululizo ilizocheza michuano hiyo. Aidha, Senegal ina kumbukumbu nzuri kwenye michuano ya mwaka 2002 Korea Kusini na Japan ilipocheza mechi mbili na kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Uruguay na kutinga hatua hiyo, leo wanaweza kurudia jambo hilo? Kila la kheri kwao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com