Polisi katika wilaya ya Pader nchini Uganda wamemkamata mwanaume mwenye miaka 30 baada ya kumpiga mtoto wake wa miaka 7 kwa fimbo mpaka kufa kisa tu mtoto huyo amekataa kwenda shule.
Richard odokonyero mwenye miaka 7 alikuwa akisoma katika shule ya msingi Pader kabla ya uhai wake kukatishwa na baba yake Denis Omony Juni 6,2018.
Mwenyekiti wa eneo hilo Charles Otto Lalobo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa baba huyo aligeuka hayawani na kumshambulia mwanae kwa fimbo kichwani kabla ya kufariki.
Inadaiwa kuwa mtoto huyo aligoma kwenda shule kwa kile alichokidai kuwa anatendewa vibaya na mama yake wa kambo na alikuwa akimuomba baba yake ampeleke kwa bibi yake akaishi huko.
Kwa mujibu wa msemaji wa Polisi katika mkoa wa Aswa River Jimmy Patrick Okema amesema kuwa mtuhumiwa huyo ameshikiliwa katika kituo cha Polisi cha Pader na atashitakiwa kwa kosa kuua punde tu upelelezi ukikamilika.
Social Plugin