Baba mzazi wa aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson, Joe Jackson enzi za uhai wake.
Baba mzazi wa aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson mzee Joe Jackson amefariki Dunia kwa ugonjwa wa Saratani (Cancer) akiwa na umri wa miaka 89 jana Jumatano.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka nchini humo vimeeleza kuwa Bw. Jackson alikuwa akipambana na saratani ya kongosho .
Inadaiwa kuwa kwa miaka mingi, Jackson ambaye alizaliwa Julai 26, 1928, huko Fountain Hill, Arkansas alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya afya.
Joe alikuwa mzazi aliyefanikiwa sana kusimamia watoto wake katika historia ya muziki ambapo aliweza kujenga kundi la The Jackson 5, na kisha baadaye Michael na Janet Jackson kama wasanii solo.
Amefariki dunia ikiwa imepita siku moja tangu kumbukumbu ya miaka tisa ya kifo cha mwanae Michael ambaye alifariki dunia Juni 25 2009.
Jackson alikuwa na watoto 10 pamoja na Katherine ambaye ni mke wake wa zaidi ya miaka 60.
Social Plugin