Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BINTI AUAWA KWA KUKATWA PANGA NA BABA YAKE MASAA MACHACHE KABLA YA HARUSI YAKE

Binti Oyinye Aguluka ameuawa kwa kukatwa na panga na baba yake mzazi, Cletus Aguluka, masaa machache kabla ya harusi yake.

Binti huyo ambaye anaishi nchini Nigeria yalimkuta masahibu hayo akiwa amelala usingizini, baada ya baba yake aliyekuwa amelewa kuja na panga na kumshambulia.

Mama Mzazi wa marehemu aliyetambulika kwa jina la Georgina amesema mume wake alirudi usiku akiwa amelewa na kuwauliza watoto wake mahali ilipo tochi yake, lakini hakuna ambaye alimjibu kutokana na kwamba walikuwa wameshaingia kulala, na ndipo alipokuja na panga na kuanza kumshambulia binti yake huyo ambaye alitakiwa kufunga ndoa Jumamosi hii ya Juni 2, 2018.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na wazee wa kijiji na kupelekwa kituo cha polisi, ambako anashikiliwa mpaka sasa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com