Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DHARAU WABUNGE KUPIMA SAMAKI WALIOPIKWA YAMCHEFUA SPIKA NDUGAI...WAZIRI AOMBA RADHI


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemshukuru Waziri wa wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kwa kitendo cha kuomba radhi na kutoa maelezo kwa kitendo maofisa wa wizara yake kuingia bungeni bila ridhaa huku Ndugai akikitafsiri kitendo cha kupima samaki kuwa kilikuwa kitendo cha dharau.

Spika ameyasema hayo mara baada Waziri Mpina kusema kilichofanyika kilikuwa sehemu ya utekelezaji wa shughuli za wizara ikiwamo operesheni sangara ambapo jana ilitendeka bungeni lakini kwa bahati mbaya utekelezaji huo haukuzingatia tararibu za Bunge.

Akipokea taarifa hiyo Spika amesema “Tumshukuru waziri kwa maelezo aliyoyatoa, lakini kwa waziri mkuu tunasikitishwa sana na kilichotokea, sisi si Bunge pekee duniani, sisi ni jumuiya ya kimataifa, wenzetu wakisikia kuna waziri na maofisa walichofanya ni dharau ya juu sana,”amesema.

Spika Ndugai ameongeza kwamba “Wapimaji wa wizara wanapima samaki mikono haina hata gloves, mikono wazi, wanashika shika, si wao peke yao, wamealika na waandishi wa habari, yaani ni kama mpango fulani wa kuliweka Bunge kusipostahili, kwa kawaida naomba tukubaliane nami, ukiwa umekasirika sana unapaswa kusamehe,”.

Hata hivyo Waziri Mpina amekiri kuwa aliona samaki wa sato akahisi wapo chini ya sentimita 25 katika mgahawa wa Bunge ndipo alipoamua kuagiza maofisa wake.

“Napenda kukiri kwamba watumishi katika kutekeleza kazi hiyo waliingia bila kibali, kupima chakula kilichopikwa na kwa taratibu hizo, wizara inaliomba radhi Bunge lako tukufu na wewe mwenyewe.” Mpina. 

Mbali na hayo Spika ameanisha kwamba linapotokea kosa la jinai katika eneo la Bunge, Kamanda wa polisi ana wajibu wa kumjulisha Spika.
Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com