Timu ya taifa ya England imeibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya timu ya taifa ya Panama, kwenye mchezo wa Kundi G uliomalizika jioni hii huko Urusi.
Ushindi huo umeacha rekodi mbalimbali ambapo mshambuliji wa timu hiyo na klabu ya Tottenham Harry Kane amefunga 'Hat-trick' yake ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Sasa amefikisha mabao 5 na kuwa mbele ya Cristiano Ronaldo na Romelo Lukaku wenye mabao 4 kila mmoja.
Mbali na rekodi hiyo pia timu ya taifa ya England imefikisha mabao 8 kwenye fainali za mwaka huu, ambayo ni idadi kubwa ya mabao tangu ilipofunga idadi hiyo katika fainali za mwaka 1954 na 1990. Idadi kubwa ya mabao kuwahi kufungwa na England kwenye Kombe la dunia ni mabao 11 mwaka 1954.
Harry Kane pia ndio mchezaji wa tatu wa England kufunga Hat-trick kwenye Kombe la Dunia akitanguliwa na Geoff Hurst mwaka 1966 na Gary Lineker mwaka 1986 dhidi ya Poland.
England pia imefunga mabao kuanzia manne kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo kwenye fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1966 dhidi ya Ujerumani ambapo ilitwaa ubingwa. England na Ubeligji zimetinga hatua ya 16 bora kutoka Kundi G.
Social Plugin