Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HOUSE GIRL AUA MTOTO MCHANGA KISHA KUUA BOSI WAKE

Mfanyakazi 'House Girl' mmoja wa ndani amemuua mwajiri wake Elizabeth Achieng pamoja na kichanga chake chenye miezi mitatu huko Kisumu nchini Kenya.

Imedaiwa kuwa mfanyakazi huyo alianza kwa kumpiga mtoto mpaka akamuua kisha akamfuata mama yake na kumchoma kisu mara kadhaa na kisha kumchoma na kitu kinachodhaniwa kuwa ni pasi ya umeme au tindikali.

Kwa sasa jeshi la Polisi Kisumu linamtafuta mfanyakazi huyo ambaye ametokomea sehemu isiyojulikana.

Taarifa zinasema kuwa katika tukio hilo mfanyakazi huyo hakumgusa binamu wa marehemu aliyekuwepo eneo la tukio.

Aidha inasemekana kuwa mfanyakazi huyo alikuwa anaendana kiumri na mwajiri wake kitu kilichokuwa rahisi kwa yeye kutekeleza tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com