Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

INSTAGRAM YAZINDUA MFUMO MPYA WA VIDEO NDEFU WA IGTV KAMA YOUTUBE

Ikiwa utawaalika watumiaji wakuu wa mtandao wa Instagram kwa warsha, ni vyema uhakikishe kuwa warsha hiyo inaweza kuwafaa.

Mfumo mpya wa video ndefu inayosimama ambao utaanza kutumika kwenye mtandao wa Instagram na ambao utakuwa na app yake ni muhimu sana kwa kampuni mzazi Facebook.

Vijana wanaiona Facebook kama mtandao unaowafaa wazazi au babu zao.

Ndio sababu wao huelekea kwa Snapchat au YouTube kuweza kupata huduma za mitandao.

Hawapendi video zinazotengenezwa kwa kutumia mfumo wa zamani lakini baadala yake hutafuta mambo yaliyo na mahanjamu.

Kwa mfumo wa IGTV, Instagram sawa na vile imefanya awali, imenakili teknoljia ambayo tayari imefumbuliwa na wengine. Inaaamini kuwa matumizi yake makubwa na fedha ilizo nazo vitaiwezesha kuwa mshindi.

Instagram tayari imenakili mfumo wa Snapchart ambapo watumiaji huchapisha watakacho ni kilichochapishwa hutoweka baada ya siku moja.

IGTV haitakuwa na matangazo ya biashara lakini mkuu wa Instagram Kevin Systrom anasema hilo litabadilika karibuni.

Matangazo ya biashara ya video yana mapato ya juu kuliko matangazo mengine yote ya mitandaoni.

Huduma hiyo mpya ya IGTV inafanikisha mikakati ya kuweza kupata sehemu ya pato hilo.

Facebook iko nyuma ya Youtube kwa watumiaji wa kati ya miaka 18 na 24 ambao matangazo ya biashara huwalenga zaidi.

Instagram nayo inaweza kuwa nyuma lakini watumiaji wake bado wanazidi kuongezeka.

Hatma ya IGTV inategemea sana iwapo manyota wa Instagram na wengine wataweka jitihada zaidi katika kuunda video za kusimama.

Kwa kuanza IGTV haitawalipa wale wanaochapisha video lakini hata hivyo huenda ikawalipa ikiwa matangazo ya biashara yatawekwa.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com