Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Muliro, ametoa ufafanuzi wa Jeshi la Polisi kuhusu Mwalimu wa Shule ya Msingi ya St Florence iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Ayoub anayedaiwa kuwadhalilisha kingono wanafunzi wake wa kike wanne kwa kuwaingilia huku akimpapasa mwanafunzi wake mwingine.
Kamanda Muliro amesema jeshi la polisi limeanza kufanya uchunguzi juu ya suala hilo kwa kushirikiana na wanafunzi hao wanne wanaodaiwa kuingiliwa na ‘mwalimu Ayoub’ na uchunguzi utakapokamilika watamfikisha mtuhumiwa mahakamani.
Aidha, Kamanda Muliro amesema jeshi la polisi pia linaendelea kumtafuta mtuhumiwa anayedaiwa kukimbia baada ya taarifa za tukio hili kusambaa na kwamba hajaripoti shuleni hapo tangu Mei 24 mwaka huu.
Jana, Wabunge waliihoji Serikali kuhusu hatua gani imechukua baada ya kuwepo kwa taarifa za mwalimu huyo kufanya kitendo hicho kichafu kwa watoto ambapo Waziri Jenister Mhagama alisema Serikali inalifanyia kazi na itaeleza Bungeni hatua gani imechukua baada ya uchunguzi kukamilika.
Social Plugin