Kampuni ya kimataifa ya Regus, ambayo inajihusisha na kupangisha ofisi za kisasa za muda na za kudumu imefungua kituo kipya cha nne cha ofisi za kupangisha jijini Dar es Salaam.
Jengo jipya la ofisi za Regus kwa ajili ya matumizi ya kupangisha ofisi zisizo na usumbufu wa masharti liko eneo la Msasani Penisula, na linazo ukubwa wa mita za mraba 590 kwa ajili ya matumizi ya ofisi za kisasa.
“Tumefungua jengo la nne la kituo cha biashara lenye maeneo ya ofisi za kupangisha,hii ni fursa pekee kwa Mashirika Yasio ya Kiserikali,na makampuni ya kimataifa kujipatia sehemu za ofisi za kisasa. Eneo hili la biashara limelenga makundi yote ikiwemo wajasiriamali wanaoanza biashara kwa kuwa bei zake za pango ni za kawaida na rahisi kuzimudu” ,alisema Joanne Bushell,Meneja wa Regus nchini.
Regus imepanua huduma zake kutokana na ongezeko la mahitaji ya ofisi kwa matumizi mbalimbali na kwa gharama nafuu bila kuhangaika kununua samani za ofisi, kuingia mikataba ya kipindi cha muda mrefu na kulipia huduma mbalimbali za matumizi ya ofisi kama umeme na maji.
Kituo hicho cha biashara cha Regus kinazo ofisi za kupangisha, kumbi za mikutano zenye huduma mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya uhakika kupitia mtandao wa internet na simu za mezani, majiko na sehemu za kupumzikia, huduma za usafi, huduma za mapokezi na utawala.
Kampuni inao mpango wa kuendelea vituo vingine vya biashara katika siku za usoni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya ofisi zisizo na masharti na usumbufu,Regus inaendesha vituo vya biashara katika miji ipatayo 900 kwenye nchi zaidi ya 120 duniani,ikiwa inahudumia wajasiariamali wa kawaida, watu binafsi na makampuni makubwa ya kimataifa.