Seneta wa Australia aliyezaliwa nchini Kenya Lucy Gichuhi amejikuta kwenye wakati mgumu kaika vyombo vya habari baada ya kushtakiwa kwa kutumia fedha za walipa kodi kwa biashara isiyo rasmi.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 56 ameshtakiwa kutumia dola 2139 (Ksh.216, 327) sawa na pesa za kitanzania 4879272 kusafirisha ndugu zake wawili kutoka Darwin kwenda Adelaide, Australia, kwa ajili ya sherehe yake ya siku ya kuzaliwa.
Mfuko uliotumiwa na Bi. Gichuhi unasemekana kuwa unatumiwa na Wabunge wa bunge la Australia wakati wa kusafiri kwa kazi rasmi na kulipa wajumbe wa familia ili kujiunga nao katika bunge au uchaguzi.
"Mbali na vyombo vya habari kuripoti kuhusu gharama zangu za kusafiri, hili lilikuwa kosa la utawala linalohusisha kutokuelewa sheria za kusafiri. Nimeagiza idara kunipatia 'invoice' ili kulipia $2139".