Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella akizungumza baada ya MV.Mwanza kushushwa majini
***
Kivuko kipya na cha kisasa cha MV.Mwanza kimeshushwa rasmi hii leo Jumapili Juni 17,2018 katika maji ya Ziwa Victoria kwa ajili ya kukamilisha hatua za mwisho za ukarabati kabla ya kuanza kufanya kazi.
Viongozi na wananchi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe.John Mongella, wameshuhudia tukio hilo na kutoa pongezi kwa serikali na kampuni ya Songoro Marine Transport kwa ujenzi wa kivuko hicho.
“Hatujamaliza hata miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano lakini vitu vinavyofanyika utadhani tuna miaka 10 tayari na kwa jinsi Mhe.Rais anavyotupeleka tutakuwa mbali sana baada ya miaka 10”,amesema Mhe.Mongella.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Songoro Marine Transport, Saleh Songoro amesema kivuko hicho kitakuwa tayari kufanya kazi baada ya wiki tatu baada ya kushushwa majini.
Kivuko cha MV.Mwanza kimegharimu shilingi bilioni 8.9 na kina uwezo wa kubeba tani 250 ambazo ni sawa na magari 36 na abiria 1000 ambapo wananchi wamefurahishwa na ujio wa kivutko hicho wakisema kitasaidia kurahisha huduma za usafiri katika eneo la Kigongo-Busisi, Ziwa Victoria.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Social Plugin