Kijiji cha Hokse nchini Nepal kimebatizwa jina la ‘Kidney Village’ baada ya asilimia kubwa ya raia wake wanaoishi kwenye kijiji hicho kuwa wameuza Figo zao kutokana na hali duni ya maisha.
Inadaiwa kuwa Wakazi wa Kijiji hicho hali zao za kiuchumi ni duni sana kitu kinachowasukuma kuingia katika biashara ya kuuza figo zao ili wapate fedha za kujikimu katika maisha ya kila siku.
Kwa upande mwingine madalali wanaofanya biashara hiyo ya figo wametajwa kuzunguka sana katika kijiji hicho na kuwashawishi Wanakijiji hao kuuza figo zao, ili na wao wapate ahueni ya maisha.
Aidha familia hizo inasemekana husafiri hadi Hospitali moja huko nchini India ili kutolewa Figo zao na kulipwa zaidi ya shilingi Milioni 3 za Kitanzania, ambazo huwa fedha za muda mfupi na baadae huanza kuteseka tena.
Social Plugin