Jamaa mmoja ambaye ni mwanafunzi mjini Eldoret nchini Kenya amewashangaza watu wengi baada ya kushika headlines kwa kuunda gari linalotumia Nishati ya jua (Solar), sasa saivi amegundua kitanda kinachozalisha umeme kutokana mtikisiko wa kitanda hasa wakati wa kujamiiana.
Samuel Karumbo, anayesomea stashahada ya mambo yanayohusu Umeme katika chuo cha Kitale National Polytechnic alisema kuwa kitanda hicho kiliundwa ili kutumia mtikisiko wowote wa kitanda hasa wakati wa kufanya mapenzi.
Karumbo amesema jinsi watu wanapojamiiana mara nyingi, ndivyo wanavyozalisha nguvu nyingi za umeme.
Amesema kuwa alitumia gharama ya KSh 2,000 ambazo ni sawa na shilingi 45000 za Tanzania ila akakiuza kwa KSh 4,000 (90000) na amekuwa akipata wateja wengi wanaohitaji vitanda hivyo.