Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBOWE ATOKA HOSPITALI ALIKOLAZWA

Afya ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili imeimarika na ameruhusiwa kutoka hospitali huku akieleza kuwa kilichokuwa kikimsumbua ni msongo wa mawazo na uchovu kupita kiasi.


Mbowe ambaye ni Munge wa Hai na Kiongozi Mkuu wa CHADEMA ameweka hayo wazi wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari waliofika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo Jijini Dar es salaam.

Mbowe amesema afya yake ni nzima hadi sasa, baada ya kumaliza msiba ataendelea kufanya vipimo maalumu vya kiafya kwa kadiri ambavyo atatakiwa na madaktari wake kama itakuwa ndani au nje ya nchi.

Mbowe pia amewashukuru viongozi wa vyama mbalimbali pamoja na watanzania ambao walimtembelea na hata waliokuwa wakimuombea kwa njia mbalimbali katika kipindi hiki yeye na familia yake ikiwa na wale ambao walizuiwa kumuona kutokana na sheria za kitabibu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com