Katika hali ya mshangao mkubwa na isiyokuwa ya kawaida miche ya bangi imebainika ikiwa imeoteshwa katika viwanja vya bunge nchini Japan jijini Tokyo.
Miche hiyo ya bangi iling'olewa baada ya kugundulika na watu waliotembelea jengo hilo, ingawa haijafahamika mara moja miche hiyo ilioteshwa lini na nani.
Afisa mmoja wa bunge la nchi hiyo amesema kuna uwezekano mbegu za bangi zilipeperushwa na upepo au kinyesi cha ndege wa angani na kuota katika bustani ya bunge .
Japan ni nchi yenye sera ya kutovumilia matumizi ya dawa za kulevya na mtu anayekamatwa na dawa hizo hata kwa kiwango kidogo hukumu yake ni kifungo jela miaka mitano.
Chanzo-BBC
Social Plugin