Msemaji wa Jeshi nchini Kanali Ramadhan Dogoli amesema kuwa, miili ya Askari 12 wa JKT akiwemo mmoja wa JWTZ, waliofariki kwa ajali Jijini Mbeya inatarajiwa kuagwa kesho katika kikosi cha JKT Itende, Jeshi kugharamia usafiri kupeleka miili ya marehemu makwao.
Akizungumza na wanahabari jijini Mbeya, Kanali Dogoli amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi uliopelekea gari kukatika ‘break’ kutokana na mteremko mkali katika eneo la Igodima na kuangukia korongoni.
“Miili ya marehemu inatarajiwa kuagwa kesho katika kikosi cha JKT Itende, Jeshi litagharamia usafiri kupeleka miili ya marehemu makwao”, amesema Kanali Dogoli.
Askari hao walipata ajali iliyosababishwa na mwendokasi uliopelekea gari kupoteza muelekeo na kuangukia korongoni, mnamo Juni 14 katika eneo la Igodima jijini Mbeya wakati wakitokea mkoani Tabora.
Social Plugin