Hatimaye timu zilizokuwa zikiliwakilisha Bara la Afrika, katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi zimeondolewa katika hatua ya makundi ambapo Senegal imekamilisha kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Colombia.
Yerry Mina ameitoa Senegal Kombe la Dunia licha ya sare kati ya pande hizo kutosha kuwawezesha wawili hao kushiriki hatua ijayo ya muondoano.
Beki huyo wa Barcelona na Colombia, Mina, alitia kichwa kimiani dakika ya 74 na kuwavunja moyo mashabiki wa Senegal ugani Samara.
Colombia wamemaliza viongozi wa Kundi H, Japan ikitoka ya pili.
Kombe la Dunia kuendelea bila timu ya Afrika hatua za mchujo!
Ingawa Japan imelazwa na Poland, imefuzu kutokana na rekodi nzuri ya nidhamu.
Bara la Afrika ambao hutoa mataifa matano katika kila michuano ya Kombe la Dunia, liliwakilishwa na nchi za Tunisia, Nigeria, Morocco, Senegal na Misri kwani hizo ndio timu zilizokuwa zimefuzu, lakini michuano ya 2018 ndio kwa mara ya kwanza mataifa manne ya kiarabu kwa pamoja yalishiriki michuano hiyo Misri, Tunisia, Morocco na Saudi Arabia.
Senegal ambayo imekubali kipigo kutoka kwa Colombia imekamilisha michezo kwa kundi H, ambapo wataaga michuano hiyo pamoja na Poland ambao walikuwa wakikamilisha ratiba japo wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Japan.
Vilevile Tunisia ambao tayari wameshayaaga mashindano watakuwa wanacheza ili kukamilisha ratiba, dhidi ya Panama kwenye mchezo kundi G, mechi ikianza saa 3 kamili usiku.
Social Plugin