Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MOTO WATEKETEZA MITIHANI NA VYETI VYA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI KAZIMA TABORA


Picha haihusiani na tukio halisi

Jengo la utawala la shule ya sekondari Kazima katika Manispaa ya Tabora limeteketea kwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyaraka mbalimbali ikiwemo mitihani ya kujipima, ya kidato cha nne na cha tano.

Akizungumza na wanahabari Mkuu wa shule hiyo Mrisho Kivuruga, amesema jengo hilo limeanza kuungua na moto majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo.

Kivuruga amesema moto huo umeteketeza nyaraka zote muhimu za shule hiyo ikiwemo vyeti vya wanafunzi, mitihani ya kujipima uwezo iliyomalizika juzi, chumba cha zahanati, vitabu na vifaa mbalimbali vilivyokuwemo katika jengo hilo na ofisi zake zote.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Suzan Nyarubamba amesema, kufuatia kuteketea mitihani hiyo uongozi wa Mkoa utasimamia ili wanafunzi hao warudie mitihani yao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com