Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MSAFARA WA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA WAPATA AJALI...KUNA TAARIFA YA KIFO

Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James umepata ajali katika eneo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu leo Jumapili Juni 10, 2018.

Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Boniventure Mushongi amesema ni kweli ajali hiyo imetokea lakini anasubiri kupatiwa ripoti kamili.

“Ni kweli taarifa za awali zinasema hivyo, inasemekana kuna basi limeligonga gari lao kwa nyuma” amesema Mushongi.

Katika Ukurasa wake wa Facebook Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ameandika ujumbe ufuatao.
SAD NEWS;-Msafara wa Mwenyekiti wa UVccm Taifa Comrade Kheri James umepata ajali akiwa Wilayani Meatu-Ambapo Diwani wa Kata ya TindaBuligi Mr.Seleman Mahega amepoteza maisha akiwa Hospital ya Mwandoya alipokuwa akipatiwa huduma ya kwanza,Madiwani 4 ambao wamepata majeraha taratibu za kuwapeleka Hospital ya Rufaa Bugando kwa matibabu na uchunguzi zaidi zinafanyika-Natoa Pole nyingi sana kwa Familiya ya Marehemu,wananchi wa kata ya Tindabuligi,viongozi wa chama na serikali Wilaya ya Meatu kwa kuondokewa na moja ya viongozi ambao walijitoa sana kuwatumikia wananchi wao-MUNGU AMPE PUMZIKO LA MILELE Ndugu yetu Mahega,Tunawaombea pia waliopata majetuhi-Baba yetu wa Mbinguni-Awape uponyaji Majeruhi wote waweze kurejea katika afya zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com