Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ambaye ameongezeka katika orodha ya wavumbuzi wa magari ya nishati ya jua na uvumbuzi huo umekuwa kivutio katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Samuel Karumbo, mwenye umri wa miaka 30, ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Kitale Polytechnic, amevumbua gari hilo katika mji wa Langas Eldoret. Gari hiyo yenye siti mbili na matairi manne lina jopo (panel) la nishati ya jua kwa nyuma.
Baadhi ya taarifa za gari hilo ni pamoja na Kutoa 0% ya uchafuzi wa mazingira, Jina la gari hilo ni SOLAR CAR. Gari hilo linasemekana kuwa na uwezo wa kutembea kufikia kilomita 50 kwa siku likiwa limejaa chaji.