Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jila la Josephine Peter (51)mkazi wa Mrara kata ya Mamire wilayani Babati mkoani Manyara ameuawa na watu wasiofahamika huku shingo yake ikikatwa na kitu chenye ncha kali.
Kamanda wa polisi mkoani Manyara Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema mwanamke huyo alifariki dunia Juni 19,2018 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake na mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kutokana na mauaji hayo.
Kamanda amesema kuwa hadi sasa chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika kwani mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kubainika kuwa hajabakwa kama watu wanavyozusha bali jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo la mauaji amesema kuwa ukikamilika taarifa kamili itatolewa
Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara).
Na Vero Ignatus , Manyara.
Social Plugin