Picha haihusiani na tukio
Ndege ndogo ya abiria iliyokuwa ikitokea mjini Kitale kwenda Nairobi iliyoripotiwa kupotea nchini Kenya mapema wiki hii imepatikana katika msitu wa Ababea huku watu 10 waliokuwa kwenye ndege hiyo wakiwa wamefariki dunia.
Kufuatia tukio hilo, Rais wa nchini humo Uhuru Kenyatta kupitia ukurasa wake maalum wa twitter amesema amehuzunika kusikia ajali ya hiyo ya ndege ndogo kuangua kutoka na hitilafu katika eneo la Kinangop.
Mbali na hilo, Rais Uhuru ameishukuru timu ya ufuatiliaji na ukoaji kutoka Mamlaka ya ndege ya Kenya kwa kuweza kulishughulikia jambo hilo kwa ukaribu sana na hatimaye kupata majibu yaliyokuwa yanastahili kwa kila mmoja kufahamu kilichotokea.
Social Plugin