Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NIGERIA YAWA TIMU YA PILI KUPATA ALAMA TATU KUTOKA AFRIKA....NI BAADA YA KUITANDAIKA ICELAND BAO 2-0

Dakika 90 za mchezo wa kundi D umemalizika kwa Nigeria kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Iceland.


Mechi hiyo imekuwa ya pili kwa timu kutoka Afrika kupata ushindi baada ya Senegal kuitwanga Poland 2-1 katika mchezo wa kundi H.

Mabao yote ya Nigeria yamewekwa kimiani na Ahmed Mussa katika dakika za 49 na 75.


Ushindi huo sasa unawaweka pazuri Nigeria na kuwapa imani Argentina kuwa wanaweza kufuzu hatua ya 16 bora kwani kufuzu kwa Argentina na Nigeria kutatokana na timu zote mbili kupata ushindi zitakapo kutana June 26 ila Nigeria hata sare inamvusha hatua inayofuata.

Croatia tayari amefuzu hatua ya 16 kutokana na kupata ushindi mechi mbili na kuwa na point 6, wakati Nigeria wao wapo nafasi ya pili kwa kuwa na point tatu, Iceland nafasi ya tatu kwa kuwa na point moja sawa na Argentina walio nafasi ya nne kwa kutofautiana magoli ya kufungwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com