Kampuni ya Uchimbaji wa madini ya Acacia inayomiliki mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu imezindua rasmi maonyesho ya Mashindano ya Kombe la dunia yanayoendelea Urusi katika uwanja wa Halmashauri ya mji Kahama mkoani Shinyanga.
Akizindua maonesho hayo,Jana Juni 21,2018 mkuu wa wilaya ya kahama Fadhili Nkurlu ameipongeza kampuni ya Acacia kwa kuendeleza mahusiano mazuri na jamii na kuwasisitiza wadau wengine kuiga mfano wa Acacia ili kusukuma mbele maendeleo ya wilaya.
Awali akizungumza kwa niaba ya uongozi wa Acacia, mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Asa Mwaipopo,alisema wanazindua rasmi uoneshwaji wa mchezo wa kombe la dunia ambapo katika halmashauri ya mji wa Kahama itaoneshwa katika uwanja wa halmashauri ya Mji wa Kahama na katika shule ya msingi Kakola A halmashauri ya Msalala.
Kwa upande wake afisa michezo wa halmashauri ya mji wa kahama Lupola Mkomwa aliwataka wananchi kuwa wamoja katika kujenga mahusiano ya karibu na kampuni hiyo sambamba na kudumisha upendo na amani.
Kampuni ya Acacia kupitia Migodi yake ya Bulyanhulu na Buzwagi itaonyesha mashindano yote ya Michezo ya kombe la Dunia ili kutoa nafasi kwa jamii kushuhudia mashindano hayo.
Katika ufunguzi huo mchezo wa Mpira wa Miguu na mpira wa Pete ilichezwa kati ya Timu ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kahama na wafanyakazi wa kampuni ya Acacia ambapo Katika mchezo wa mpira wa Miguu Timu ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kahama ilishindi kwa Goli 1-0 dhidi ya timu ya Acacia na kwa upande wa mpira wa Pete timu ya kamati ya Ulinzi na usalama ilishinda magori 21 kwa 5 dhidi ya timu ya Acacia.
Katika hatua nyingine Kampuni ya Acacia kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu imetenga shilingi bilioni 1.2 kufadhili awamu ya pili ya ujenzi wa kituo cha afya Bugarama ambacho kikikamilika kinatarajiwa kuhudumia watu zaidi ya 150, 000 katika vijiji vinavyozunguka mgodi na maeneo jirani.
Hayo yamebainishwa na meneja mkuu wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedicto Busunzu, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo wa kuonyesha michezo hiyo.
ANGALIA MATUKIO KATIKA PICHA
Mkurugenzi wa kampuni ya Acacia Asa Mwaipopo akizungumza katika uzinduzi huo,madhumuni ya kuonyesha mubashara michuano ya kombe la dunia.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akifungua rasmi maonyesho ya kombe la dunia katika uwanja wa halmashauri ya Mji wa Kahama.
Wachezaji wa timu ya Acacia wakipeana mawili matatu na kuomba dua ili washinde katika mchezo huo.
Wachezaji wakisalamiana kabla ya kuanza kwa mtanange.
Kikundi cha burudani cha Kilema Hodi kikitumbuiza katika ufunguzi huo.
Kikosi cha timu ya Acacia kikiwa uwanjani tayari kumenyana na kikosi cha timu ya kamati ya ulinzi na usalama.
Mgeni rasmi katika mchezo huo Asa Mwaipopo akisalimiana na waamuzi kabla ya kuanza kwa mchezo.
Wachezaji wa timu ya Acacia wakipasha misuli kabla kuanza kwa mchezo huo.
Kikosi cha kamati ya ulinzi na usalama kikipasha kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akijiweka sawa kabla ya mchezo dhidi ya kamati ya ulinzi na usalama na timu ya kampuni ya mgodi ya Acacia.
Kikosi cha timu ya kamati ya ulinzi na usalama kikipeana mbinu kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Golikipa wa timu ya Acacia Elias Kasitila akipasha kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akiteta jambo na mchezaji wa timu ya acacia kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Acacia wakiwa wamewasili uwanjani tayari kwa kuanza mashindano hayo ya mpira wa pete na mpira wa miguu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akiweka viungo sawa kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama Timoth Ndanya akichua mguu kabla ya kuanza kwa mtanange dhidi ya wapinzani wao timu ya Acacia.
Dawati la ufundi la timu ya Acacia likiwa makini kufuatilia mpambano.
Dawati la ufundi la timu ya kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama likiwa makini kufuatilia mpambano.
Kipindi cha mapumziko timu ya Acacia ikibadilishana mawazo na kocha wao tayari kurudi katika kipindi cha pili.
Baadhi ya wananchi wa mji wa Kahama wakifuatilia michuano ya mpira wa pete.
Mfungaji wa timu ya kamati ya ulinzi na usalama Mage akiwa katika heka heka ya kushambulia.
Vuta nikuvute ikiendelea katika mpira wa pete kati ya timu ya kamati ya ulinzi na usalama na timu ya mgodi ya Acacia.
Mashabiki wakiwa wameketi na wengine kusimama wakishuhudia mtanange wa kukata na shoka
Mvutano mkali wa piga nikupige ukiendelea katika uwanja wa halmashauri ya mji Kahama.
Miamba ikimenyana katika mchezo huo
Mchuano ya mpira wa pete ukiendelea kati ya timu ya acacia na timu ya kamati yaulinzi na usalama.
Dawati la ufundi la timu ya Acacia wakiwa uwanjani wakishuhudia mtanange.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Golikipa wa timu ya Acacia Elias Kasitila ambaye aliibuka kuwa Man of the Match akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo
Washindi wa mchezo wa mpira wa pete wakipita mbele ya meza ya mgeni rasmi kupewa mkono wa pongezi kwa kushinda dhidi ya timu ya Acacia.
Washindi wa mpira wa miguu timu ya kamati ya ulinzi na salama wakipokea zawadi ya kitita cha shilingi laki tano.