Chama cha Wakunga Tanzania (Tanzania Midwives Association-TAMA) kimeendesha semina kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya afya ya uzazi na mtoto sambamba na elimu kuhusu ukunga na majukumu ya wakunga.
Semina hiyo imefanyika leo Jumamosi Juni 30,2018 katika ukumbi wa Submarine Hotel Mjini Kahama na kukutanisha pamoja waandishi wa habari zaidi ya 20 kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari aliwataka akina mama wajawazito kuhakikisha wanajifungulia katika vituo vya afya wakihudumiwa na wakunga wataalamu badala ya kukimbilia kwa wakunga wa jadi wasio na utaalamu wa kuhudumia mama na mtoto ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.
“Hatutaki kusikia mama na mtoto wanafariki wakati wa kujifungua,tunashauri wakunga wa jadi wawalete akina mama wajawazito kwenye vituo vya afya/hospitali lakini pia wajawazito waache tabia ya kujifungulia nyumbani kwani ni hatari kwa mama na mtoto kwa sababu mama anaweza kuvuja damu nyingi ama kupata kifafa cha mimba”,alieleza Dkt. Lebashari.
Alitoa rai kwa watoa huduma kwa mama na mtoto hospitalini kuhakikisha kuwa na utaalamu wa kutosha kwani mama mjamzito anatakiwa kupewa huduma kwa kiwango cha juu ili kulinda uhai wake na mtoto wake.
“Mkunga yeyote anatakiwa kuwa mahiri katika kuhudumia mama mjamzito,mkunga wa kweli hawezi kugombana na wateja”,aliongeza Dkt. Lebashari.
Kwa upande wake,Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini Martha Rimoy alisema waandishi wa habari ni wadau muhimu sana katika afya ya uzazi na mtoto hivyo ni vyema wakatumia vyema kalamu zao kuhakikisha huduma kwa mama na mtoto zinakuwa bora.
“Tunatoa wito kwa waandishi wa habari waihamasishe jamii kushirikiana na wakunga ili panapotokea changamoto katika kumhudumia mama na mtoto basi zitatuliwe mapema”,alisema Rimoy.
Aidha aliwaomba waandishi wa habari kuihamasisha jamii kuzingatia matumizi ya njia za uzazi wa mpango pamoja na kuchangia damu ili kusaidia changamoto ya vifo vya mama na mtoto kwani vifo vingi vinatokana na kukosekana kwa damu.
Naye Mratibu wa huduma za afya uzazi na mtoto mkoa wa Shinyanga, Joyce Kondoro alisema vifo vya mama na mtoto vinaendelea kutokea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokwa damu nyingi,kifafa cha mimba,utoaji mimba usio salama na uzazi pingamizi.
Nao waandishi wa habari waliwatupia lawama viongozi katika vituo vya afya/hospitali na serikali kwa ujumla kwa urasimu katika kutoa taarifa pale wanapohitaji kuweka katika usawa habari zao ‘kubalance story’ kwamba wamekuwa wakiwakwepa waandishi wa habari na kusingizia kuwa wao siyo wasemaji.
“Sekta ya afya inakabiliwa na changamoto nyingi,mfano wauguzi na wakunga ni wachache wanaelemewa na kazi nyingi na kushindwa kuhudumia wateja hivyo ni vyema serikali ikaangalia namna ya kuajiri wakunga wengi zaidi ili kuboresha huduma ya mama na mtoto”,walishauri waandishi wa habari.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA SEMINA
Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini Martha Rimoy akielezea malengo ya semina kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga leo Juni 30,2018 katika ukumbi wa Submarine Hotel Mjini Kahama.Picha zote na Kadama Malunde,John Mponeja na Frank Mshana
Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini Martha Rimoy akiwasisitiza waandishi wa habari kuandika habari zinazohusu huduma ya afya ya uzazi na mtoto wakati akielezea majukumu ya mkunga ambayo ni pamoja na kuhudumia akina mama wajawazito
Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini Martha Rimoy akizungumza wakati wa semina hiyo.
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akiwahasisha waandishi wa habari kuandika habari kuhusu wakunga wataalamu na kuibua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika masuala ya afya uzazi na mtoto
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akiwaomba waandishi wa habari kuihamasisha jamii kushirikiana na wakunga ili kuhakikisha mama na mtoto wanapata huduma bora
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akizungumza ukumbini
Mwandishi wa habari wa Star TV, Shaban Allei akichangia hoja ukumbini
Mwandishi wa habari gazeti la Habarileo Kareny Masasy akiuliza swali wakati wa semina hiyo.
Waandishi wa ha habari wakiwa ukumbini
Mkurugenzi wa Malunde1 blog Kadama Malunde1 blog,Kadama Malunde (katikati) akiandika dondoo muhimu wakati wa semina hiyo.
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu wakati wa semina hiyo
Waandishi wa habari wakifuatilia mada ukumbini
Semina inaendelea
Mratibu wa huduma za afya uzazi na mtoto mkoa wa Shinyanga, Joyce Kondoro akielezea kuhusu hali ya huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoani Shinyanga hadi Desemba 2017
Mratibu wa huduma za afya uzazi na mtoto mkoa wa Shinyanga, Joyce Kondoro akifafanua jambo ukumbini
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akielezea namna ya kuhudumia mama mjamzito anapojifungua ili kuhakikisha hapotezi maisha yeye na mtoto
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari na Mratibu wa Chama cha Wakunga nchini Martha Rimoy wakionesha kwa vitendo namna mtoto anavyokuwa wakati wa kuzaliwa na jinsi inavyoweza kutokea akapoteza maisha wakati wa kutoa huduma wakati wa kujifungua endapo mama hatahudumiwa na mkunga mtaalamu
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akisisitiza kuwa watoa huduma lazima wawe mahiri katika kuhudumia akina mama wajawazito ili kuepusha vifo vya mama na mtoto
Waandishi wa habari wakifuatilia mada kwa umakini
Katibu wa Chama cha Wakunga nchini, Dkt. Sebalda Leshabari akiendelea kutoa somo kwa vitendo
Waandishi wakifuatilia mada ukumbini
Semina inaendelea
Picha ya pamoja washiriki wa semina hiyo
Picha ya pamoja
Picha zote na Kadama Malunde,John Mponeja na Frank Mshana
Social Plugin