Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro leo Ijumaa Juni 1,2018 amekabidhi msaada wa nguo za shule na kadi za bima ya afya kwa wanafunzi 200 wanaoishi katika mazingira magumu katika kata za Chamaguha,Ibadakuli,Kizumbi, Mwawaza na Mwamalili zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.
Msaada huo umetolewa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la mjini Shinyanga linalotoa huduma za kijamii kwa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza.
Akizungumza wakati wa Tamasha lililokwenda sanjari na ugawaji wa sare za shule na kadi za bima ya afya,Matiro alisema bado wilaya yake inakabiliwa na changamoto ya mimba na ndoa za utotoni huku miongoni mwa sababu zinachochangia ikiwa ni ugumu wa maisha.
“Lazima wadau na kila mmoja katika jamii ashiriki katika kukabiliana na changamoto zinazosababisha watoto wetu wapate mimba na wengine kuolewa wakiwa shuleni,na pale inapotokea kuna mtu anataka kurubuni mtoto basi aripotiwe mara moja”,alisema Matiro.
Aidha alilishukuru shirika la TVMC kwa kazi nzuri linazofanya katika kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuyataka mashirika mengine kuendelea kuwafikia zaidi wananchi ambao wanaishi katika mazingira magumu.
“Niwashukuru sana kwa sare za shule na kadi za bima ya afya kwani bima ya afya ndiyo mkombozi wa afya ya mwananchi,bila afya bora hatuwezi kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda”,alisema Matiro.
“Sisi kama serikali hatuwezi kufanya majukumu yote hivyo lazima tushirikiane na sekta binafsi hivyo niyashukuru mashirika na taasisi mbalimbali ambazo zinaendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi”,aliongeza.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo kuwatahadharisha baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakishirikiana na wanaotia mimba wanafunzi na kumaliza kesi kinyemela na kubainisha kuwa itafikia kipindi serikali itaanza kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wanaochangia kugandamiza watoto wa kike.
Alisema ili kumkomboa mtoto wa kike ni lazima jamii ibadilike na kila mmoja kuwa tayari kukemea vitendo viovu wanavyofanyiwa watoto.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Jonas Ngangala alisema wanafunzi waliopata msaada huo wanatoka katika mazingira magumu na kwamba shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali katika kuwafikia watu wanaohitaji msaada.
“Tamasha hili la TVMC lililenga kutoa zawadi kwa mabalozi wetu 200 kutoka shule na kata mbalimbali za Manispaa ya Shinyanga,wanaohusika kuzuia mimba na ndoa za utotoni kwa watoto wenzao, tumetoa kadi za bima ya afya ‘Kadi za uanachama wa CHF’ na sare za shule kwa wanafunzi hawa ili kuwapa hamasa wasirubunike na wanaume walaghai wanaoweza kuwapatia ujauzito”,alieleza.
“Pia tumepoa asante kutoka kwenye vikundi vya wazazi wa Manispaa ya Shinyanga tulivyokuwa tunafanya navyo kazi za Kijasiriamali ambavyo tumeviwezesha kuanzia ngazi ya chini kabisa na sasa vimeweza kujitegemea na kufanya shughuli zao za kijasirimali kwenye maeneo yao”,aliongeza
Ngangala alisema shirika lake limetoa jumla ya shilingi 600,000/= kuwezesha vikundi vya akina mama wajasiriamali ili kuwainua kiuchumi waweze kulea familia zao vizuri na kuwezesha wanafunzi kwenda shule.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza wakati wa Tamasha la TVMC lililokwenda sanjari na utoaji wa msaada wa nguo za shule na kadi za bima ya afya kwa wanafunzi 200 wanaoishi katika mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akiwasisitiza wanafunzi kuepuka vishawishi ili waweze kumaliza masomo yao na wazazi kuwajibika kulea watoto vizuri na kuhakikisha wanawapeleka shule.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akiendelea kuzungumza wakati wa tamasha la TVMC.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akiwataka wazazi na walezi kuacha tabia ya kurubuni watoto waolewe na kumaliza kienyeji kesi za wanaume wanaotia mimba wanafunzi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akiendelea kuzungumza wakati wa tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Jonas Ngangala akielezea namna shirika hilo linavyoshirikiana na serikali katika kuwafikia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Jonas Ngangala alisema wameamua kutoa kadi za bima ya afya kwa watoto ili kuunga mkono serikali ya awamu ya tano inayotaka wananchi wake wawe na afya bora kwa ajili ya kufikia uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Mussa Jonas Ngangala akizungumza wakati wa tamasha hilo la TVMC
Afisa Elimu Sayansi Kimu na Afya Manispaa ya Shinyanga,Beatrice Mbonea akizungumza wakati wa tamasha hilo ambapo alilishukuru shirika la TVMC kutoa msaada wa sare za shule na kadi za bima ya afya kwa wanafunzi 200 waliopo katika manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya kadi za bima afya walizopatiwa wanafunzi 200 waliopo katika manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akishikana mkono na mmoja wa wanafunzi wakati wa zoezi la kugawa kadi za bima ya afya watakazozitumia kwa ajili ya matibabu
Mwanafunzi akishikana mkono na Katibu wa siasa na uenezi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Rajabu Bwanga baada ya kupata kadi yake ya bima ya afya.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akimvalisha sare za shule mwanafunzi,wakati wa zoezi la kugawa sare za shule kwa wanafunzi 200 wanaoishi katika mazingira magumu katika manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akikabidhi sare za shule kwa mmoja wa wanafunzi hao.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akimvalisha sare za shule mwanafunzi.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yan
Mmoja wa wazazi waliopo katika vikundi vilivyoundwa na shika la TVMC akisoma risala,pamoja na mambo mengine alilishukuru shirika hilo kuwawezesha kuunda kikundi na sasa wanaendeleza wao wao wenyewe vikundi vyao.
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Dotto Joshua akilishukuru shirika la TVMC kwa kutoa sare za shule na kadi za bima za afya kwa wanafunzi hao na kuyaomba mashirika mengine kujitokeza na kusaidia wananchi wanaoshi katika mazingira magumu.
Diwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya akizungumza wakati wa tamasha la TVMC
Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Shinyanga Mjini,Rajabu Bwanga akizungumza wakati wa Tamasha la TVMC na kulishukuru shirika la TVMC kuwafikia wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Hussein Egobano akizungumza wakati wa tamasha la TVMC.
Mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao,Richard Masule akitoa neno la shukrani kwa shirika la TVMC.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog