Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela leo Ijumaa Juni 1,2018 amefunga mafunzo ya siku tatu kwa wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Investing in Children and their Societies (ICS – Africa).
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga alisema ili kukomesha vitendo hivyo ni lazima kila mmoja ashiriki kwa nafasi yake.
“Ni lazima wadau wote waweke nguvu ya pamoja kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,hivyo mafunzo haya mliyopata yawe chachu ya kuleta mabadiliko katika jamii yetu ili wanawake na watoto waishi salama”,alieleza Msovela.
Aidha alisema kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga ni kamati ya kwanza nchini kuundwa na kupatiwa mafunzo na tayari uundaji wa kamati katika ngazi ya halmashauri,kata na vijiji unaendelea.
Mafunzo hayo yaliyoanza Mei 30,2018 yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kukutanisha wajumbe wa kamati hiyo ambao kwa pamoja watashiriki katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga.
Kupitia mafunzo hayo,wajumbe wa kamati hiyo wamejifunza kuhusu dhana ya masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto lakini pia wamejifunza maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifunga mafunzo hayo.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisisitiza jambo ukumbini.
Afisa Mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto kutoka shirika la ICS mkoa wa Shinyanga,ambao ndiyo wafadhili wa mafunzo hayo,Shadia Nurdin akiwashukuru wajumbe kuhudhuria mafunzo hayo na kuwaomba kwenda kufanyia kazi mambo waliyojifunza kwa muda wa siku tatu ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbia akiwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuendelea kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Kulia ni Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la kuhudumia watoto la Save the Children mkoa wa Shinyanga Alex Enock akiteta jambo na Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Shinyanga,Bahati Mwaipasu wakati wa mafunzo hayo.
Afisa Mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto kutoka shirika la ICS mkoa wa Shinyanga,Shadia Nurdin akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.Kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga,Lydia Kwesigabo.
Picha ya pamoja wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga.
Picha ya pamoja wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog