Shirika la Thubutu Africa Initiatives (TAI) ni shirika lisilo la kiserikali limetambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kwa viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga ili waweze kuufahamu mradi na kufundishwa mbinu za utekelezaji wa mradi huo.
Mradi huo umetambulishwa leo Ijumaa Juni 22,2018 katika ukumbi Empire Hotel mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam.
Awali akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo, Mkurugenzi wa Shirika la Shirika la Thubutu Africa Initiatives lenye makao yake makuu mjini Shinyanga,Jonathan Kifunda alisema mradi huo utatekelezwa katika kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga.
“Tumekutana hapa kutambulisha mradi huu kwa viongozi wa ngazi ya kata sambamba na kuwatambulisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii (watatu kila kata) ambao kimsingi ni watakelezaji wa mrad huu watakaofanya kazi katika kila kata”,alieleza Kifunda.
Alisema Shirika la Thubutu Afrika Initiatives linatekeleza mradi wa USAID Tulonge Afya katika kata 17 za manispaa ya Shinyanga chini ya ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia mashirika la Fhi360 na T- Marc Tanzania.
Alibainisha kuwa Mradi wa Tulonge Afya ni mradi wa afya unaolenga kuelimisha jamii ili kubadili tabia za watu katika jamii waweze kutumia vituo vya afya,zahanati,hospitali pale inapohitajika,kuhamasisha watu wengi zaidi kupima VVU/UKIMWI na kushawishi watu wanaoishi na VVU/UKIMWI kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU.
Aidha alisema mradi huo pia unalenga kuibua watu wenye maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI pamoja na kifua kikuu na kuwaunganisha na huduma za afya za karibu.
Naye Afisa Mawasiliano Mabadiliko ya Tabia mradi wa USAID Tulonge Afya mkoa wa Shinyanga ,Mgalula Ginai alisema mradi huo unaofadhiliwa na Watu wa Marekani, mkoani Shinyanga unatekelezwa katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga na Mji Kahama.
Alisema mradi huo utakaodumu kwa miaka mitano unatarajiwa kufikia malengo ya asilimia 90 tatu “90,90,90” zinazolenga kuhakikisha asilimia 90 ya watu wanaohisiwa kuwa na maambukizi wanapima afya,kutumia ARVs na kufubaza makali ya VVU.
“Mradi huu unaosimamiwa na shirika la Fhi360 na wadau mbalimbali kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania unaenda sanjari na utekelezaji wa kampeni ya Pima na tibu mapema ‘Test and Treat All Campaign’ inayojulikana kama ‘Furaha Yangu’ yenye lengo la kuhimiza upimaji wa VVU na utumiaji wa dawa mapema pale mtu anapobainika kuwa na maambukizi ya VVU",alieleza Mgalula.
"Mradi wa USAID Tulonge Afya unashughulika na uhamasishaji na utoaji wa elimu katika maeneo makuu matano ambayo ni: elimu ya kupunguza maambukizi ya VVU,uzazi wa mpango, kifua kikuu, malaria na afya ya mama na mtoto na kwa upande wa elimu na uhamasishaji wa kupunguza maambuzi ya VVU kwa sasa mradi unaendesha kampeni ya Test and Treat "Furaha Yangu" kwa lengo la kufikia 90 tatu na kauli mbiu ya kampeni hii ni 'Pima,Jitambue,Ishi",aliongeza Mgalula.
"Mradi wa USAID Tulonge Afya unashughulika na uhamasishaji na utoaji wa elimu katika maeneo makuu matano ambayo ni: elimu ya kupunguza maambukizi ya VVU,uzazi wa mpango, kifua kikuu, malaria na afya ya mama na mtoto na kwa upande wa elimu na uhamasishaji wa kupunguza maambuzi ya VVU kwa sasa mradi unaendesha kampeni ya Test and Treat "Furaha Yangu" kwa lengo la kufikia 90 tatu na kauli mbiu ya kampeni hii ni 'Pima,Jitambue,Ishi",aliongeza Mgalula.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam aliwataka wananchi kuacha uoga wajitokeze kupima afya zao na pale wanapobainika kuwa na maambukizi ya VVU basi waanze kutumia dawa.
Imeandikwa na Kadama Malunde - Malunde1 blog
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives (TAI) likitambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kwa viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives (TAI) likitambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Kifunda ,kulia ni Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Magedi Magezi.
Mkurugenzi wa Shirika la Shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Kifunda akizungumza wakati wa kutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kwa viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa Shirika la Shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Kifunda akielezea kuhusu namna shirika hilo lilivyojipanga kutekeleza mradi wa USAID Tulonge Afya.
Mkurugenzi wa Shirika la Shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Kifunda akiwaomba viongozi wa kata na wahudumu wa afya kushirikiana na shirika hilo katika kutekeleza mradi wa USAID Tulonge Afya
Viongozi wa kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii wakiwa ukumbini
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Magedi Magezi akizungumza wakati wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives (TAI) likitambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kwa viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga
Wadau wa afya wakiwemo viongozi wa kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii wakiwa ukumbini
Viongozi wa kata wakiwa ukumbini
Maafisa kutoka Shirika la Thubutu Africa Initiatives wakiwa ukumbini
Viongozi mbalimbali wakiwa ukumbini
Afisa Mawasiliano Mabadiliko ya Tabia mradi wa USAID Tulonge Afya mkoa wa Shinyanga ,Mgalula Ginai akielezea kuhusu mradi huo wakati wa kutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kwa viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga
Afisa Mawasiliano Mabadiliko ya Tabia mradi wa USAID Tulonge Afya mkoa wa Shinyanga ,Mgalula Ginai akiwahamasisha viongozi wa kata na wadau wote wa afya kuielimisha na kuihamasisha jamii kupima afya
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikata utepe ishara ya kutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kwa viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam, Mkurugenzi wa Shirika la Shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Kifunda ,kulia ni Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Magedi Magezi wakipiga makofi baada ya zoezi la kukata utepe ishara ya kutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kwa viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga
Viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Meneja Miradi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Paschalia Mbugani akielezea zaidi kuhusu Mradi wa USAID Tulonge Afya.
Viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga wakifuatilia matukio ukumbini
Viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Viongozi wa kata na wahudumu wa afya ngazi ja jamii wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini...
Viongozi wa ngazi ya kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin