Shirika la Internews kwa kushirikiana na shirika la USAID Tulonge Afya na Fhi360 limeendesha warsha kwa waandishi wa habari mikoa ya Shinyanga na Mwanza wanaozalisha vipindi na habari zenye maudhui ya afya kwa ajili ya kuwajengea uwezo namna ya kuandika habari sahihi zinazohusu afya.
Warsha hiyo ya siku moja imefanyika Juni 21,2018 katika ukumbi wa Jb Belmonte Hotel Jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza, Dk. Pius Masele aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo,Dk. Masele aliwataka waandishi wa habari kutumia vyema mafunzo hayo ili waweze kuandika kwa usahihi habari zinazohusu masuala ya afya hususani masuala ya VVU na UKIMWI.
“Waandishi wa habari mna nafasi kubwa ya kuielimisha jamii kuhusu VVU/UKIMWI,tunaamini kabisa kupitia kampeni ya Furaha Yangu ambayo ipo ndani ya Mradi wa USAID Tulonge Afya iliyozinduliwa hivi karibuni nchini mtaweza kuandika habari sahihi ili kuihamasisha jamii kupima afya”,alieleza Dk. Masele.
Dk. Masele aliwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuhamasisha jamii kubadili tabia ili kupunguza maambukizi ya VVU.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Shirika la Internews Wenceslaus Mushi alisema mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kuandika habari za afya bila kupotosha jamii ili wananchi waweze kubadili tabia na kuwa na jamii yenye afya bora.
Naye Meneja wa USAID Tulonge Afya kanda ya Magharibi na Ziwa ,Sihiana Mkanda aliwasihi waandishi hao wa habari kuandika habari kutumia taaluma yao vizuri kufikia malengo ya 90 90 90 ili kuhakikisha watu wanapima VVU, kutumia dawa na kufubaza makali ya VVU.
"Kwa mujibu wa shirika la Umoja waMataifa la Mpango wa Kupambana na Ukimwi Duniani ifikapo 2020, asilimia 90% ya watu wenye maambukizi ya VVU watafikiwa na kupimwa,ambapo asilimia 90% ya walioathirika watapewa dawa za kufubaza virusi (antiretroviral treatment) na kwamba asilimia 90% ya watakaotumia dawa hizo hawataweza kuwaambukiza wenza watakaojamiiana nao kwasababu virusi vitakuwa vimefubazwa na tiba hiyo", Mkanda alifafanua kuhusu 90 tatu.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza, Dk. Pius Masele akifungua semina kwa waandishi wa habari mikoa ya Mwanza na Shinyanga kuhusu namna ya kuandika habari za afya katika ukumbi wa JB Belmonte Hotel jijini Mwanza
Mratibu wa Kudhibiti Ukimwi mkoa wa Mwanza, Dk. Pius Masele akifungua semina kwa waandishi wa habari mikoa ya Mwanza na Shinyanga kuhusu namna ya kuandika habari za afya
Waandishi wa habari mikoa ya Mwanza na Shinyanga wakiwa ukumbini
Mafunzo yanaendelea
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Shirika la Internews Wenceslaus Mushi akielezea kuhusu mradi wa Boresha Habari unaolenga kuwajengea uwezo wa waandishi wa habari kuhusu namna ya kuandika habari za afya kwa usahihi
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Shirika la Internews Wenceslaus Mushi akiwasisitiza waandishi wa habari kuandika habari kwa usahihi
Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu wakati wa semina hiyo
Mafunzo yanaendelea
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Meneja wa USAID Tulonge Afya kanda ya Magharibi na Ziwa akielezea kuhusu mradi wa Tulonge Afya
Meneja wa USAID Tulonge Afya kanda ya Magharibi na Ziwa akielezea kuhusu kampeni ya Pima na tibu 'Test and Treat all campaign'
Meneja wa USAID Tulonge Afya kanda ya Magharibi na Ziwa akisisitiza jamba ukumbini
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Waandishi wa habari walioshiriki mafunzo kuhusu habari za afya wakiwa katika picha ya pamoja na watoa huduma za afya hususani VVU na UKIMWI kutoka vituo vya afya wilaya ya Nyamagana na Sengerema ambao pia wamehudhuria mafunzo kuhusu masuala ya afya.
Waandishi wa habari walioshiriki mafunzo kuhusu habari za afya wakiwa katika picha ya pamoja na watoa huduma za afya hususani VVU na UKIMWI kutoka vituo vya afya wilaya ya Nyamagana na Sengerema ambao pia wamehudhuria mafunzo kuhusu masuala ya afya.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog