Mtuhumiwa wa ujambazi anayedaiwa kuteka magari na kunyang'anya mali za watu wanaotumia barabara ya Kisili - Buhigwe mkoani Kigoma maarufu kwa jina la ‘Rambo’ ameuawa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Ottieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mtuhumiwa huyo ameuawa akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Wilaya Kasulu kutokana na kipigo alichopata kutoka kwa wananchi wenye hasira.
"Kwa kuwa tumehamasisha jamii kumkabili huyo Rambo kwa vile anatumia bunduki za bandia, watu walipomuona waliamua kumkabili na wakamdhibiti kikamilifu kabla ya kutupigia simu,"amesema Kamanda Ottieno
Rambo alikuwa raia wa Burundi anayetoka jimbo la Makamba, lakini aliingia Kigoma kwa njia za panya kinyume cha sheria na alikuwa akitumia bunduki bandia zilizochongwa kwa ustadi akitumia mbao na kuviringisha vitambaa ili kuwahadaa watu anaowateka alikuwa tishio kutokana na kuwakwepa polisi mara mbili.
CHANZO- EATV
CHANZO- EATV
Social Plugin