Shule ya sekondari ya Wasichana ya Moi nchini Kenya imefungwa kwa dharula kwa muda wa wiki moja, baada ya kuwepo kwa tuhuma za vitendo vya ubakaji.
Katibu wa Tume ya Elimu Amina Mohamedi ametoa agizo la kufungwa kwa shule hiyo Juni 3,2018 baada ya kufanya kikao na uongozi wa shule hiyo, ambayo imekutwa na tukio la ubakaji.
Katibu huyo amesema kwamba serikali inajipanga kuweka ulinzi shuleni hapo, huku ikijiandaa kufanya hivyo kwa shule zingine ili kuzuia vitendo kama hivyo visijitokeze tena.
Shule ya hiyo ambayo hivi karibuni ilikumbwa na tukio la ajali ya moto, imekumbwa na tukio la ubakaji baada ya mtu mmoja kuingia bwenini na kubaka wanafunzi watatu.
Social Plugin