Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wamewatambulisha wachezaji wake watatu wapya ambao watawatumia katika michuano iliyo mbele yao ikiwemo Kombe la Kagame litakaloanza leo.
Wachezaji waliotambulishwa na Simba mbele ya waandishi wa habari ni Serge Wawa Pascal 'Ramos', Mohammed ‘Meddie’ Kagere kutoka Gor Mahia na Deogratius Munishi ‘Dida’ kutoka Pretoria University ya Afrika Kusini.
Akiwatangaza wachezaji hao, Afisa habari wa Simba, Haji Manara amesema nyota hao wamesajiliwa kwa kuzingatia timu yao msimu ujao itashiriki michuano mingi.
“Nawatangaza wachezaji hawa kwenu ili umma uweze kuwafahamu na hawa wamesajiliwa ili kuiongezea nguvu timu yetu msimu ujao, tumemsajili Meddie, Dida na Wawa ili kuongeza upana wa kikosi chetu”, amesema Manara.
Manara ameongeza kuwa “Hatutaki kusajili watu wa maneno mengi, huyu Meddie wakati tunacheza mechi ya fainali kule Kenya tukiwa kwenye korido kabla ya kuingia uwanjani, niliongea maneno ya shombo ili kuwatoa mchezoni Gor Mahia.
Aidha Manara amesema kuwa, klabu imewasajili wachezaji wengine watatu ambao ni Marcel Kaheza kutoka Majimaji, Adama Salama kutoka Lipuli na Mohammed Rashida wa Prisons ya Mbeya.
Social Plugin