Klabu ya Besiktas imetozwa faini na Uefa baada ya Paka kujitosa uwanjani wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich mwezi Machi mwaka huu.
Mwamuzi Michael Oliver alisimamisha mchezo katika kipindi cha pili cha mchezo uliochezwa Vodafone Park mpaka mnyama huyo alipoondoka katika dimba hilo.
Klabu hiyo ya Uturuki wameshutumiwa kwa uratibu usiokidhi viwango na wamepigwa faini kutokana na vitendo vya mashabiki kurusha vitu uwanjani na kufunga njia za kwenye ngazi, na kusababisha kutozwa faini ya pauni (£29,880).
Besiktas ilimaliza kwa ushindi wa 8-1 kwa wingi wa magoli ya kufunga kisha kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali, huku mashabiki wa klabu hiyo ya Ujerumani ikipiga kura kuwa Paka ni mchezaji bora wa mchezo huo.
Social Plugin