Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Mitrovic mnamo dakika ya 5 tu ya mchezo kwa upande wa Serbia huku la Switzerland likiwekwa kimiani na Granit Xhaka mnamo dakika ya 52 kabla ya Xherdan Shaqiri kuongeza msumari wa mwisho dakika ya 90 ya mchezo
Xhaka ambaye hivi karibuni amesaini mkataba wa muda mrefu kuitumikia Arsenal ameweka rekodi ya kupiga jumla ya pasi 71 ambazo hazijapigwa na mchezaji yoyote wa Urusi katika michuano hiyo tangu 1996.
Matokeo hayo yanaifanya Uswizi kuwa pointi sawa na Brazil katika kundi E lakini ikishika namba 2 kutokana na idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Social Plugin